CHUO CHA KWANZA CHA MUSA,
GHALIBU HUITWA
GENESIS,
AU
MWANZO WA MWENYIEZI MNGU KUUMBA
IHapo mwanzo Mwenyiezi Mngu
aliumba hizo mbingu na hii nti.
2 Na nti ilikuwa haina sura, tena ilikuwa
ni tupu hamuna kitu ndani yakwe ; na
katika uso wa uziwa palikuwa na kiza :
na roho wa Mwenyiezi Mngu akatulia
juu ya uso wa hayo maji. 3 Mwenyiezi
Mngu akasema, Na uwe muanga : ukawa
muanga. 4 Na Mwenyiezi Mngu aka-
uona huo muanga, kuwa ni mwema :
Mwenyiezi Mngu akapambanua muanga
na kiza. 5 Mwenyiezi Mngu akauita
huo muanga Mtana, na hicho kiza aka-
kiita Usiku. Kukawa na jioni, kukawa
na asubuhi, siku moja.
6 Mwenyiezi Mngu akasema, Na liwe
anga kati ya hayo maji, illi lipambanue
maji haya na haya. 7 Mwenyiezi Mngu
akalifanya lile anga, na kuyapambanua
hayo maji yaliyokuwa tini ya anga na
hayo maji yaliyokuwa juu ya anga :
ikawa vivyo. 8 Na Mwenyiezi Mngu
akaliita lile anga Mbingu. Kukawa na
jioni, kukawa na asubuhi, siku ya pili.
9 Mwenyiezi Mngu akasema, Maji haya
yaliyo tini ya mbingu na yatangamani-
shwe pahali pamoja, ipate kuwa wazi ile
nti kavu : ikawa vivyo. 10 Mwenyiezi
Mngu akapaita pale pakavu Nti, na mata-
ngamano ya maji akayaita Bahari : na
Mwenyiezi Mngu akayaona kuwa ni
mema. 11 Mwenyiezi Mngu akasema,
Nti na imee nyasi, na mboga, iletayo
mbeyu, na mti wenyi matunda uzaao
SWAHILI O.T.
matunda kwa aina zakwe, ambayo mna
. mbeyu yakwe ndani yakwe, juu ya nti :
ikawa vivyo. 12 Nti ikamea nyasi, na
mboga iletayo mbeyu kwa aina zakwe,
na mti uzaao matunda, ambayo mna
mbeyu yakwe ndani yakwe, kwa aina
zakwe : Mwenyiezi Mngu akaona kuwa
ni mema. 13 Kukawa na jioni, kukawa
na asubuhi, siku ya tatu,
14 Mwenyiezi Mngu akasema, Na iwe
mianga katika anga la mbingu, ipate
pambanua mtana na usiku ; nayo iwe ni
ishara, na nyakati, na siku, na myaka :
15 tena iwe mianga katika anga la
mbinguni kuleta muanga juu ya nti :
ikawa vivyo. 16 Mwenyiezi Mngu aka-
f anya hiyo mianga miwili mikubwa ; ule
mkubwa sana kutamalaki mtana, na ule
mdogo wakwe kutamalaki usiku : aka^
fanya na zile nyota pia. 17 Mwenjdezi
Mngu akaitia hiyo mianga katika anga la
mbinguni ipate leta muanga juu ya nti,
18 na kutamalaki juu ya mtana na juu
ya usiku, na kupambanua muanga na
kiza : Mwenyiezi Mngu akaona kuwa ni
mema. 19 Kukawa na jioni, kukawa na
asubuhi, siku ya-ne.
20 Mwenyiezi Mngu akasema, Hayo
maji na yajawe ni ungi-ungi wa nyama
wenyi uhai, nyuni nao na wapuruke juu
ya nti katika naf asi ya anga la mbinguni.
21 Mwenyiezi Mngu akaumba mingumi
mikuu, na killa nyama mwenyi nafusi na
uhai mwenyi kutapatapa majini, ambao
1. 22—2. 19.
GENESIS
hayo maji yalijawa nao ungi-ungi, kwa
aina zakwe, na killa nyuni mwenyi ma-
bawa kwa aina zakwe : Mwenyiezi Mngu
akaona kuwa ni mema. 22 Mwenyiezi
Mngu akawabarikia, huku akisema, Zaani,
muongezeke sana na kuyajaza hayo maji
katika bahari, nyuni nao na waongezeke
juu ya nti. 23 Kukawa na jioni, kukawa
na asububi, siku ya tano.
24 Mwenyiezi Mngu akasema, Nti na
izae nyama mwenyi nafusi na uhai kwa
aina zakwe, hayawani, na wadudu, na
nyama wa nti, kwa aina zakwe : ikawa
vivyo. 25 Mwenyiezi Mngu akamfanya
nyama wa nti kwa aina zakwe, na haya-
wani kwa aina zakwe, na killa mdudu juu
ya nti kwa aina zakwe : Mwenyiezi Mngu
akaona kuwa ni mema. 26 Mwenyiezi
Mngu akasema, Natumfanye mtu kwa
sura zetu, kwa mfano wetu : na wawe
na enzi juu ya samaki walio baharini, na
juu ya nyuni walio angani, na juu ya
hayawani, na juu ya nti yo'e, na juu ya
killa mdudu mwenyi kutarabaa juu ya
nti. 27 Mwenyiezi Mngu akamuumba
mtu kwa sura zakwe, kwa mfano wa
Mwenyiezi Mngu ndivyo alivyomuumba ;
mume na mke akawaumbi. 28 Mwe-
nyiezi Mngu akawabarikia ; Mwenyiezi
Mngu akawambia, Zaani, muongezeke,
muijaze nti, na kuitawala iwe tini yenu ;
iwani na enzi juu ya samaki walio ba-
harini, na juu ya nyuni walio angani, na
juu ya killa kilicho na nafusi na uhai
kiendacho juu ya nti. 29 Mwenyiezi
Mngu akawambia, Angaliani, Niraewapa
nyinywi killa mboga iletayo mbeyu, iliyo
juu ya uso wa nti yote, na killa mti ambao
una tunda la mti ndani yakwe liletalo
mbeyu : kwenu nyinywi kitakuwa ni
chakula : 30 tena killa nyama wa nti, na
killa nyuni wa angani, na killa kitu kita-
mbaacho juu ya nti, kilicho chenyi nafusi
na uhai, nimewapa killa mboga yenyi
majani mabiti kiwe chakula chao : ikawa
vivyo. 31 Mwenyiezi Mngu akakiona
killa kitu alichokuwa amekifanya, nacho
ni chema sana. Kukawa na jioni, kuka-
wa na asubuhi, siku ya sita.
2Basi mbingu na nti zilikwisha fany wa
pamoja na jeshi yakwe yote. 2 Ka-
tika siku ya sabaa Mwenyiezi Mngu aka-
maliza kazi yakwe aliyokuwa ameifanya ;
nae akapumzika siku ya sabaa na kuiata
ile kazi yakwe yote aliyokuwa ameifanya.
3 Mwenyiezi Mngu akaibarikia ile siku
ya sabaa na kuitakasa : kwa kuwa katika
siku hiyo akapumzika na kuiata kazi
yakwe yote ambayo Mwenyiezi Mngu
alikuwa ameumba na kuifanya.
4 Hivi ni vizazi vya mbingu na vya nti
hapo zilipoumbwa, katika siku hiyo
ambayo Jehova Mwenyiezi Mngu alizi-
fanya mbingu na nti. 5 Wala mti hau-
tasa kuwa juu ya nti hata mmoja, na
majani ya barani hayajamea, kwa kuwa
Jehova Mwenyiezi Mngu hajanyesha
mvua juu ya nti, wala hapakuwa na mtu
kuifanya kazi ile nti : 6 ukazuka umande
juu ya nti ukanwesha uso wa nti wi)te.
7 Jehova Mwenyiezi Mngu akamtanya
Adamu wa udongo wa nti, kisha akamvu-
via myanzini mwa pua yakwe pumzi za
uhai ; basi Adamu akawa nafusi yenyi
uhai. 8 Kisha Jehova Mwenyiezi Mngu
akafanya busitani huko upande wa ma-
shariki, katika Eden ; akamweka huko
huyo Adamu aliyekuwa amemiinanga.
9 Jehova Mwenyiezi Mngu akaraeza kati-
ka nti killa mti upendezao kuonekana
kwakwe, na ule ulio mwema kwa chakula ;
na mti wa uhai nao katikati ya busitani,
na ule mti wenyi kuleta ujuzi wa mema
na mabaya. 10 Palikuwa na mto ulio-
kuwa ukitoka katika Eden kuinwesha ile
busitani, kutoka hapo ukagawanyikana
ukawa ni mikuno mine. 11 Jina la huo
wa kwanza waitwa Pishon : nao ni huo
ulioizingira nti nzima ile ya Havilah,
ambapo papatikana dhahabu ; 12 na
dhahabu ya nti ile ni nzuri : bedola ziko
na vito vile vya akiki ya rangi ya chani-
kiwiti, 13 Na jina la ule mto wa pili
waitwa Gihon : nao ni huo ulioizingira
nti nzima ile ya Kushi. 14 Na jina la
huo mto wa tatu waitwa Hidekela : nao
ni huo upitao upande wa mashariki wa
Suriata. Na mto wa-ne ni huo uitwao
Earati. 15 Jehova Mwenyiezi Mngu aka-
mtwaa huyo Adamu, nae akamweka
katika ile busitani ya Eden, illi aifanye
kazi na kuituaza. 16 Na Jehova Mwe-
nyiezi Mngu akamuusia huyo Adamu,
akamwambia, Killa mti ulio katika busi-
tani una rukhusa kula utakavyo : 17
lakini ule mti wa kujua mema na mabaya,
usile matunda yakwe ; kwani katika siku
hiyo utakayoyala matunda yakwe hakika
yako utakufa. 18 Jehova Mwenyiezi
Mngu akasema. Si vyema huyo Adamu
kuwa peke yakwe ; tamfanyia msaada
mfano wakwe. 19 Jehova Mwenyiezi
GENESIS
2. 20—3. 20.
Mngu akatinanga-finanga killa nyama wa
bara kutoka katika udongo, na killa
iiyuni wa angani : nae akamletea Adamu
nyama hao, illi aone jinsi atakavyowaita :
na jina lolote Adamu alilomtaja killa
nyama mwenyi uhai, likawa jina lakwe
hilo. 20 Huyo Adamu akawapa ma jina
hayawani wote, na nyuni wa angani, na
killa nyama wa bara, lakini hakuonekana
mmoja mwenyi kumfaa huyo Adamu
kuwa msaada mfano wakwe. 21 Basi
Jehova Mwenyiezi Mngu akamlaza Adamu
katika usingizi mzito, nae akalala ; nae
akatwaa mfupa mmoja katika mbavu
zakwe, tena akapajaza nyama pahali
pakwe : 22 na ule mfupa wa mbavu
ambao Jehova Mwenyiezi Mngu alikuwa
ameutwaa katika huyo Adamu, akaufanya
mwanamke, akamleta kwa huyo Adamu.
23 Huyo Adamu akasema, Basi huyu ni
mfupa wa mifupani mwangu, na nyama
katika nyama ya muwili wangu : ataitwa
jina lakwe mwanamke, kwa sababu
alitwaliwa katika mwana-mume. 24 Kwa
ajili ya hayo mtu mume atawaata baba-
akwe na mamaakwe, nae atashikamana
na mkewe : nao watakuwa ni muwili
mmoja. 25 Nao walikuwa tupu wote
wawili huyo Adamu na mkewe, nao hawa-
kuona haya.
Q Basi huyo nyoka alikuwa ni mwenyi
•3 hila kuliko nyama wa bara awae yotc
aliyeumbwa ni Jehova Mwenyiezi Mngu.
Nae akasema na huyo mwanamke,
akamwambiay Ati, Mwenyiezi Mngu ame-
sema, Hamtakula katika miti ya busitani
yoto ? 2 Huyo mwanamke akamwambia
nyoka. Tun;', rukhusa ya kula ya matunda
ya miti ya busitanini : 3 lakini katika
matunda ya mti huo ulio katikati ya
busitani Mwenyiezi Mngu • ametwambia,
Msile matunda yakwe, wala msiuguse,
msije mkafa. 4 Na huyo nyoka aka-
mAvambia, Hakika yenu hamtakufa :
5 kwa kuwa Mwenyiezi Mngu ajua ya
kwamba katika siku hiyo mtakayokula
ya mti huo, mato yenu yatafumbuka,
nanywi mtakuwa kama waungu, kwa
kujua mema na maovu. 6 Basi hapo
huyo mwanamke alipoona ya kwamba
mti huo ulikuwa ni mwema kwa kula, tena
ya kwamba ulikuwa wapcndeza matoni,
tena ya kwamba ulikuwa ni mti wa kuta-
maniwa kumwerevusha mtu, akatwaa
katika hayo matunda yakwe, akala,
akampa na mumewe pamoja nae, nae
akala. 7 Mara mato yao hao wote
wawili yakafumbuka, wakatambua ya
kuwa wa tupu ; basi wakashona-shona
majani ya mtini, wakajifanyia wenyewe
nguo. 8 Kishawakasikiasautiya Jehova
Mwenyiezi Mngu akienda masia busi-
tanini wakati wa kuvuma upepo wa
mtana ; na huyo mtu mume na mkewe
wakajifita mbali na uso wa Jehova
Mwenyiezi Mngu kati ya miti ya busi-
tanini. 9 Jehova Mwenyiezi Mngu aka-
mwita Adamu, akamwambia, U wapi ?
10 Nae akajibu, Nilisikia sauti yako
busitanini, nami nilikucha, kwa kuwa
nilikuwa tupu ; basi nikajiiita. 11 Nae
akamuuliza, N nani aliyekwambia ya
kwamba u tupu ? Jee, umekula mti huo
niliokwambiausile ? 12 Adamu akajibu,
akisema, Huyo mwanamke uliyenipa
wewe kuwa pamoja nami, yeye ndiye
aliyenipa ya mti huo, nami nikala.
13 Jehova Mwenyiezi Mngu akamuuliza
huyo mwanamke, N neno gani hili ulilo-
fanya ? Mwanamke akajibu, akasema,
Huyo nyoka alinidanganya, nami nikala.
14 Jehova Mwenyiezi Mngu akamwambia
huyo nyoka, akisema, Kwa kuwa ume-
fanya neno hili, umelaaniwa wewe kuliko
hayawani wote, na kuliko killa nyama wa
bara ; utatambaa kwa tumbo lako, nawe
utakula mtanga siku zote za maisha yako :
15 nami tatia uadui kati ya wewe na
huyo mwanamke, na kati ya uzao wako
na uzao wakwe ; uo utakusheta kitwa
chako, na wewe utamsheta kisigino
chakwe. 16 Akamwambia huyo mwana-
mke, Nitazidisha sana usumbuiu wako na
kutunga mimba kwako, katika utungu
utazaa wana ; na tamaa yako itakuwa
ikimlekea mumeo, nae atatawala juu
yako. 17 Akamwambia Adamu, Kwa
.sababu wewe uraesikiza tamko la mkeo,
nawe umekula ya mti huo ambao nili-
kuusia, nikisema, Usile matunda yakwe :
hii nti imelaaniwa kwa ajili yako wewe ;
utakula viliwa vyakwe katika taabu siku
zote za maisha yako ; 18 nayo itaku-
mezea miba na mibaruti-mwitu ; nawe
utakula majani ya mashamba ; 19 katika
jasho la uso wako utakula chakula chako,
hata utakaporejea katika udongo ; kwa
kuwa ulitwaliwa mumo ; kwa kuwa wewe
u udongo, nawe utarejea mumo katika
udongo. 20 Huyo Adamu akamwita
mkewe jina lakwe Hawa ; kwa kuwa yeye
alikuwa mama ya wote walio hai.
;j
3. 21—5. 1. GENESIS
21 Jehova Mwenyiezi Mngu akawafanyia
Adamu na mk«^we mavao ya ngovi
akawavika.
22 Jehova Mwenyiezi Mngu akasema,
Huyu Adamu amekuwa kama swiswi
mmojawapo, mwenyi kujua mema na
mabaya ; asende akanyosha mkono
wakwe, na kutwaa ya mti wa uzima nayo,
akala, na kuishi milele : 23 kwa ajiii ya
hayo Jehova Mwenyiezi Mngu akamtoa
katika busitani ya Eden, illi ailime hiyo
nti ambayo alitwaliwa mumo. 24 Basi
akamfukuza huyo Adamu akamtoa nde ;
nae akaweka Makherubu upande wa
mashariki wa ile busitani ya Eden, na
umemetufi;! wa upanga uliokuwa walekea
huku na huku, illi kuilinda ile ndia ipele-
kayo kwenyi huo mti wa uzima.
^
AJ^U^.^.i^^
HICHI NI
CHUG KITAKATIFU CHA MWENYIEZI MNGU
KIITWACHO
MAAGANO YA KALE
MANENO YA KISAWAHILI
LONDON
BRITISH AND FOREIGN BIBLE SOCIETY
1914